FAHAMU: Vigezo vitatu (3) ambavyo Diamond Platinumz huzingatia katika kuchagua mwenza wake

Kwa mujibu wa kipindi cha Tv cha masuala ya Fashion cha Nirvana toka EATV, kimeripoti kuwa msanii maarufu wa Bongo Fleva Naseeb Abdul alimaarufu kama "DIAMOND PLATINUMZ" raisi wa WCB hupendelea vigezo vitatu vikuu katika kuchagua mwenza;
1. Awe mweupe mwenye lijishepu
2. Awe anapenda rangi ya Pink
3. Mashuhuri mwenye vijisenti
Vigezo hivi vimetolewa baada ya picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha Diamond akiwa na Boss Lady Zari wa Uganda wakila raha ufukweni.
Kwa haraka haraka kupitia wadada ambao walishawahi date na Diamond kama vile Wema Sepetu, Penny, Jokate pamoja na Zari Boss lady wote wana vigezo hivyo in common.


No comments