NEWS ALERT: Mambo nyuma ya pazia juu ya ujambazi Mohans


Mnamo majira ya jioni siku ya alhamisi wiki iliyopita. Majambazi watatu wenye silaha walivamia duka la vileo liitwao Mohans, lililopo kwa Nyerere Mikocheni wakiwa na pikipiki tatu (3) alimaarufu kama boda boda aina ya "BOXER" ambapo, walifanikiwa kuondoka kiasi cha pesa kisichojulikana. Baada kumweka mlinzi wa duka hilo chini ya ulinzi na mwingine akizuia mlango wa kutokea na mwingine wa tatu akiwa kwenye pikipiki. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa majambazi hayo kwa mara ya kwanza walikuwa wakifuatilia dada mmoja ambaye alikuwa na kiasi cha dollar 100,000 amabaye alikuwa akielekea Bureau de change, na baada ya kumpora dada huyo ndipo wakapitia katika duka ya Mohans kufanya uhalifu mwingine. Polisi waliwasili eneo la tukio baada ya majambazi kutokomea kusiko juliana

No comments