VIDEO PREMIER: 13 - Yung Killa feat. Fid Q & Belle 9


Ile video iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na yenye matarajio mengi kutoka kwa rapa Yung Killa sasa ipo hewani kupitia Smart phone, Tablet, Computer au Tv yako waweza kucheck kichupa hichi kikali. 13 ndio jina la nyimbo chini ya mtarishaji mkali wa mzuki mkongwe Tanzania P funk, Belle 9 kwenye chorus akiwemo na Fid Q. Video ya hii nyimbo ilihairishwa baada ya kifo cha Geez Mabovu mwana Hip Hop mashuhuri ambae alifariki dunia siku chache zilizopita huko Iringa, na kusababisha kuhairisha release date ya video ya 13 ambayo ilkuwa itoke tarehe 13 Nov 2014, kwa mujibu wa Yung killa "MSODOKI" kupitia profile yake ya instagram alitanabaisha hivyo kwamba aliamua kusitisha utoaji wa video hiyo ili kupisha msiba. Video ya 13 imekuwa directed by Nisher, Director mkali chipukizi aliyejinyakulia tuzo za watu ya Director bora chipukizi. Nisher ametoa Teasers kibao kibao za video ya 13, na inatarajiwa kuwa video kali ya Hip Hop mpaka hivi sasa na video ya kwanza kali toka kwa Yung Killa


No comments